Mwandishi wa IQNA mjini Makka amesema, katika majlisi hiyo ya kiraa ya Qur'ani iliyoundwa na msafara wa kwanza wa wasomaji Qur'ani kutoka Iran waliokwenda kutekeleza ibada ya umra, walimu, makarii na mahufadh wa Qur'ani Tukufu, wasimamizi wa vituo vya Qur'ani nas maqarii kadhaa mashuhuri wa Iran waliwafurahisha watu waliokwenda kutufu nyumba ya Mwenyezi Mungu kwa kiraa ya aya za Qur'ani ambayo imewavutia watu wengi.
Baada ya hapo makarii wa Iran waligawana juzuu 30 za Qur'ani Tukufu na kuhitimisha Qur'ani nzima.
Katika majlisi hiyo makarii wa Kiirani pia walisoma dua, ziara na kufanya ibada ya twawafu. 1039625