IQNA

Maonyesho ya Qur’ani Iran kuanza wiki moja kabla ya Mwezi wa Ramadhani

11:07 - June 30, 2012
Habari ID: 2356415
Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran amesema awamu ya 20 ya Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani ya Tehran yataanza wiki moja kabla ya kuanza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Akizungumza na IQNA, Seyyed Mohamad Hosseini amesema nara ya maonyesho ya mwaka hii ni , ‘Qur’an, Utamaduni wa Mwamko’.
Ameelezea matumaini yake kuwa maonyesho ya Qur’ani mwaka huu na hafala zingine mshabaha zitasaidia kuinua na kudumisha utamaduni wa Qur’ani nchini Iran.
Ameongeza kuwa maonyesho ya mwaka huu yatakuwa na vitengo vipya na kiwango cha juu cha bidhaa za Qur’ani .
Hosseini amesema suala la Mwamko wa Kiislamu litapewa umuhimu mkubwa katika maonyesho ya mwaka huu. Aidha amesema katika maonyesho hayo kutakuwa na kitengo maalumu cha walio silimu.
1038098
captcha