Mashindano hayo yanafanyika kwa jina la Imam al Hafidh al Talamsani. Wanawake wanaoshiriki katika mashindano hayo pia wameanza mchuano leo wakisimamiwa na kamati maalumu ya wanawake .
Hassan Jawani ambaye ni miongoni mwa viongozi wa taasisi ya masuala ya kiutamaduni ya Harra amesema jumuiya hiyo ina lengo la kuarifisha maulamaa wasiokuwa mashuhuri wa Algeria kwa taifa la nchi hiyo na kwamba imetayarisha mashindano hayo ya Qur'ani kwa shabaha hiyo.
Mashindano hayo ya Qur'ani ya kitaifa yanafanyika katika vitengo vinne vya hifdhi ya Qur'ani nzima pamoja na tajwidi makhsusi kwa ajili ya watu wenye umri wa chini ya miaka 35, hifdhi ya nusu ya Qur'ani Tukufu kwa watu wenye umri wa miaka 23, hifdhi ya hizbu 20 kwa wale wenye umri wa miaka 15 na hifdhi ya hizbu 10 kwa wale wenye umri wa miaka 12.
Jumuiya ya Harra ya Algeria ambayo inajihusisha na masuala ya kielimu na kimalezi, ilianza kazi zake mwaka 1989 na imekuwa ikitayarisha mashindano ya Qur'ani tangu miaka 11 iliyopita. 1041136