IQNA

Binti mwenye umri wa miaka 6 ahifadhi Qur'ani nzima India

13:07 - July 02, 2012
Habari ID: 2359074
Fatuma Swaghir binti wa miaka 6 kutoka mji wa Lucknow katika jimbo la Uttar Pradesh nchini India amefanikiwa kuhifadhi Qur'ani nzima.
Binti huyo ni mwanafunzi katika Madrasa ya Darul Qur'an ar- Rahmania inayopatikana katika eneo la Gomti Naghar.
Binti huyo mdogo amefanikiwa kuhifadhi Qur'ani nzima kutokana na juhudi kubwa alizofanya baba yake mzazi Swaghir Ahmad ambaye mwenyewe pia ni hafidh wa Qur'ani. Jambo hilo limewapelekea watoto wengine wadogo wa India waingiwe na hamu ya kutaka kuhifadhi kitabu hicho cha mbinguni na hata baadhi yao wamekuwa wakisafiri na wazazi wao kutoka maeneo ya mbali nchini India ili kwenda kumtembelea binti huyo na kushuhudia kwa karibu jinsi anavyosoma hifdhi ya Qur'ani.
Baba yake binti huyo anasema anajivunia sana binti yake huyo kwa sababu katika miaka ijayo atakuwa mhudumu wa kitabu hicho kitakatifu cha Waislamu. Ameelezea matumaini yake kwamba katika siku zijazo watoto wengine wa Kiislamu wa India watafanikiwa kufikia kiwango hicho na kuwa wahudumu wazuri wa Qur'ani.
Tunakumbusha hapa kwamba sherehe maalumu ya kuenzi na kumshukuru binti huyo mdogo wa India kutokana na juhudi zake za kuhifadhi Qur'ani nzima itafanyika katika ukumbi wa mikutano ya waandishi habari katika mji wa Lucknow. 1041803
captcha