Kongamano hilo pamoja na masuala mengine litamshukuru Ravil Gaynutdin Mufti Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Mamufti wa Russia kutokana na huduma kubwa ambazo amefanyia baraza hilo na jamii nzima ya Waislamu wa Russia.
Wakati huohuo Roshan Abbas, msimamizi wa Idara ya Baraza la Mamufti wa Russia amesema kwamba kuchaguliwa mkuu mwingine wa baraza hilo, kuwasilishwa ripoti ya shughuli za miaka mitano ya baraza hilo na kuchunguzwa mapendekezo yaliyotolewa kuhusiana na mipango ya baadaye ya baraza hilo katika miaka mitano ijayo ni mambo mengine yatakayochunguzwa katika ajenda ya kongamano hilo. 1041738