Kwa mujibu wa tovuti ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Misri mashindano hayo yatafanyika katika marhala tano tofauti kwa washindani walio na umri wa chini ya miaka 25.
Washiriki watashindana katika makundi matano tofauti ya kuhifadhi Qur'ani nzima kwa kuchunga sheria za tajwidi na tartili sambamba na kufasiri juzuu ya 15 ya Qur'ani, hifdhi ya Qur'ani nzima pamoja na kuchunga sheria zilizotajwa, hifdhi ya juzuu 20 za mwanzo, juzuu 10 za mwanzo na hatimaye hifdhi ya juzuu 6 zinazofuatana kwa kuchunga sheria za tajwidi na tartil.
Waamuzi wa mashindano hayo watakuwa watu mashuhuri walio na ujuzi mkubwa katika masuala ya Qur'ani na sheria za usomaji wake.
Watu watakaoruhusiwa kushiriki kwenye mashindano hayo watatakiwa wasiwe ni maustadh wa Qur'ani, wasomaji mashuhuri wa Qur'ani, waliohitimu masomo katika Chuo Kikuu cha al-Azhar au walioshiriki katika duru mbili zilizopita za mashindano hayo.
Waandaaji wa mshindano hayo pia wamepanga mipango ya kushirikishwa vipofu na washiriki walio na umri wa chini ya miaka 12 ambapo wataruhusiwa kushiriki kwenye mashindano hayo wakiwa na mtu mmoja wa kuwaongoza.
Mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka yana lengo la kuimarisha motisha ya usomaji Qur'ani na kuwahamasisha vijana waweze kuhifadhi kitabu hicho cha mbinguni na kuweza kutekeleza mafundisho yake maishani. 1042849