IQNA

Mchango wa wanawake wa Kiislamu katika harakati za kupinga ubeberu ni wenye taathira kubwa

11:18 - July 14, 2012
Habari ID: 2367342
Khatibu wa sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran Hujatul Islam wal Muslimin Kadhim Siddiqi amesema kuwa, mchango wa wanawake wa Kiislamu katika harakati za kupambana na ukoloni na ubepari katika eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika ni jambo lenye taathira kubwa.
Vile vile ameashiria kikao cha kimataifa cha wanawake na mwamko wa Kiislamu kilichomalizika hivi karibuni hapa mjini Tehran na kusisitiza kuwa, lengo la kufanyika kwa kikao hicho ni kuwakurubisha pamoja wanawake wa Kiislamu ili kufahamu masuala ya dini yao, na kuelewa njama za maadui za kutaka kumkandamiza mwanake duniani.
Ameashiria pia umuhimu wa mwanamke haopa chini na kusema, wanawake wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni watu muhimu katika nyanja za kielimu, kijamii, kiuchumi, kisiasa na kitamaduni.
Khatibu wa sala ya leo ya Ijumaa ya hapa mjini Tehran vile vile amezungumzia vikwazo vipya vya Wamagharibi, mashinikizo na vitisho dhidi ya taifa la Iran vilivyokuwepo tangu miaka 33 iliyopita na kusema, mambo hayo hayajafanikiwa kusimamisha malengo matukufu na irada ya wananchi shupavu wa Iran.
Amesema kuwa, Iran inavigeuza vikwazo kuwa fursa muhimu kwa ajili ya maendeleo na kwamba hata vikwazo vya Wamagharibi vya wakati nchi hii ilipokuwa katika vita vya kulazimishwa, pia havikuifanya Iran isalimu amri mbele ya matakwa yao.
1051749
captcha