Aidha waandamanaji wamelaani serikali ya Uingereza kwa kuendelea kuunga mkono tawala hizo mbili katili.
Maandamano hayo ya Jumamosi yameandaliwa na Harakati ya Uhuru ya Bahrain na wanaharakati wanaopinga vita kutoka muungano wa Stop the War.
Maandamano hayo ya London yamefanyika huku utawala wa Saudi Arabia ukiendelea kuwakandamiza waandamanaji mashariki mwa nchi hiyo. Katika kipindi cha wiki moja iliyopita, Wasaudi wanne wameuawa shahidi kufuatia hujuma ya vikosi vya ufalme wa Aal Saud dhidi ya wananchi wanaoandamana kwa amani.
Aidha utawala wa kifalme wa Aal Khalifa nchini Bahrain unaendelea kuwakandamiza waandamanaji na sasa maandamano ya wapinzani yamepigwa marufuku. Pamoja na ukatili huo, Uingereza inayodai kutetea haki za binadamu inaendelea kuziuzia tawala hizo silaha za kukabiliana na waandamanaji.
1053116