IQNA

Sherehe maalumu za taklifu ya vijana wa Kiislamu zafanyika Nigeria

23:43 - July 16, 2012
Habari ID: 2370148
Sherehe maalumu za kutimu umri wa taklifu kwa vijana wa Kiislamu zilifanyika jana Jumapili katika Husseiniya ya Baqiyatullah (as) katika mji wa Zaria nchini Nigeria.
Sherehe hizo ziliandaliwa na Harakati ya Kiislamu ya Nigeria inayoongozwa na Sheikh Ibrahim Yaqub Zakzaki.
Katika sherehe hizo Sheikh Zakzaki aliwaongoza vijana hao aliofikia umri wa taklifu katika swala ya Jamaa na kisha kuwabainishia majukumu anayopasa kuyatekeleza Mwislamu katika jamii ya Kiislamu. Amewaambia vijana hao kwamba Mwislamu anapasa kuzingatia na kutekeleza kwa makini ibada ya swala katika maisha yake ya kila siku kwa sababu swala ni nguzo ya dini.
Amesema kufikia umri wa taklifu ni neema kwa kila Mwislamu kwa sababu ni kipindi cha kuingia mwanadamu katika hatua ya kupitia mitihani na majaribio ya Mwenyezi Mungu na kwamba mwanadamu huyo anapasa kufanya juhudi za kufikia ukamilifu kwa kujaribu kushinda majaribio hayo. 1054270
captcha