IQNA

Vifurushi maalumu vya mwezi wa Ramadhani kutolewa Hispania

12:56 - July 17, 2012
Habari ID: 2370798
Vifurushi maalumu vya kiutamaduni katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ambavyo vimeteyarishwa na Idara Kuu ya Kiutamaduni ya Wairani Wanaoishi Nje ya Nchi vimepangwa kutolewa kwa Waislamu wa Hispania na Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini humo.
Vifurusi hivyo vitajumuisha Qur'ani Tukufu, dua za mwezi wa Ramadhani na CD za mafunzo kwa familia za Kiislamu. Kitengo hicho cha utamaduni pia kimechapisha na kutayarisha kadi za pongezi za kuwadia mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa ajili ya kutawanywa kati ya idara za Kiislamu na shakhisa mbalimbali wa Kiislamu nchini Hispania.
Shughuli nyingine maalumu za kitengo hicho cha utamaduni katika mwezi huu wa Ramadhani zitakuwa pamoja na kuandaa chakula cha futari kwa ajili ya kutawanywa miongoni mwa Waislamu katika miji muhimu ya nchi hiyo na vilevile mawaidha yatakayotolewa na Sheikh Suheil mmoja wa wahuburi mashuhuri wa nchi hiyo.
Kwa kuzingatia kuwa Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani inasadifiana na maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds kitengo hicho pia kimeandaa semina na vikao tofauti kwa lengo la kujadili suala hilo muhimu katika ulimwengu wa Kiislamu. 1055139
captcha