IQNA

Mashindano ya kimataifa ya "picha ya umaanawi wa Ramadhani" kufanyika Dubai

15:56 - July 18, 2012
Habari ID: 2372072
Duru ya pili ya mashindano ya kimataifa ya picha zenye maudhui ya "umaanawi wa mwezi mtukufu wa Ramadhani katika nchi mbalimbali" yatafanyika Dubai kwa hisani ya Studio Basel.
Kituo cha habari la al Kanz kimeripoti kuwa, mashindano hayo yanawakaribisha watu kutoka maeneo mbalimbali ya dunia ambao wametayarisha picha zenye maudhui hiyo kwa kutumia kamera za kitaalamu au hata zilizochukuliwa kwa kutumia simu za mkononi.
Wasimamizi wa mashindano hayo wanasema picha mia moja bora zaidi zitachaguliwa na jopo la majaji na kuchapishwa katika kitabu.
Zawadi za dola elfu mbili, elfu moja na dola mia tano zimetengwa kwa ajili ya washindi wa kwanza hadi tatu wa mashindano hayo.
Jopo la majaji wa mashindano hayo litajumuisha wataalamu mashuhuri wa sanaa duniani na watazingatia zaidi ubora wa picha, ujumbe wake na uhodari wa mpigapicha hizo.
Wanaotaka kushiriki kwenye mashindano hayo wanaweza kurejea kwenye mtandao wenye anwani ifuatayo: www.capturethespiritoframadan.org, au ukurasa wa Facebook wa: www.facebook.com/RamadanPhotography. 1056236

captcha