Katika ujumbe wake, Rais Ahmadinejad ametoa wito wa umoja katika Ulimwengu wa Kiislamu.
Katika barua tafauti alizowaandikia viongozi wa nchi za Waislamu pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC, Rais Ahmadinejad ameelezea matumaini kuwa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, ulimwengu utashuhudia ‘urafiki na udugu miongoni mwa mataifa ya dunia hasa mataifa ya Waislamu.’ Aidha amesema ana matumaini kuwa dhulma na ubaguzi utafika ukingoni na dunia kushuhudia amani na usalama wa kudumu.
Rais Ahmadinejad amewatakia furaha na ufanisi Waislamu kote duniani.
1058446