Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maandamano hayo yameandaliwa na Wizara ya Awqaf huko Gaza kwa ushirikiano na Jumuiya ya Maulamaa wa Palestina.
Waandamanaji wamelaani kile walichokitaja kuwa ni mauaji ya umati ya Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar.
Aidha Wapalestina wamelaani kimya cha jamii ya kimataifa kuhusu mauaji ya Waislamu Myanmar.
Tokea mwezi Juni mwaka huu wa 2012, maelfu ya Waislamu wa kabila la Rohingya wameuawa na makumi ya maelfu ya wengine kuachwa bila makao kufuatia machafuko yaliyozuka mashariki mwa Myanmar.
Idadi ya Waislamu wa kabila la Rohingya ni karibu milioni moja kati ya watu milioni 47 katika nchi hiyo ya mashariki mwa Asia.
1059976