Kitengo hicho pia kinaonyesha picha mbalimbali za video za mauaji ya kinyama na mateso wanayofanyiwa Waislamu hao wasio na wa kuwatetea ili kuwafahamisha walimwengu machungu wanayoyapitia.
Misaada hiyo inatazamiwa kutumwa kwa Waislamu hao katika siku za Leilatul Qadr. Mwaka uliopita kitengo hicho pia kilikusanya misaada kama hiyo kwa ajili ya Waislamu waliokumbwa na njaa wa Somalia na pia waliokumbwa na janga la mafuriko nchini Pakistan.
Maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani yanayofanyika katika Muswala wa Imam Khomeini chini ya anwani ya 'Qur'ani, Utamaduni wa Mwamko' yalianza tarehe 15 Julai na yatazamiwa kuendela kwa kipindi cha karibu mwezi mmoja. 1060374