Gazeti la Libya al Youm limeripoti kuwa Jumuiya ya Ulinganiaji wa Kiislamu imesema katika taarifa hiyo kwamba vitendo vya ubaguzi wa kizazi, mauaji ya halaiki na kuwalazimisha Waislamu kuwa wakimbizi huko Myanmar vinapaswa kulaaniwa vikali. Imesema inasikitisha kuwa jamii ya kimataifa imenyamazia kimya jinai na mauaji hayo.
Taarifa hiyo imehoji: "Vipi maelfu ya Waislamu wa Myanmar wanashambuliwa, kuuawa na kulazimishwa kukimbia makazi yao na kundi moja la watenda jinai huku jamii ya kimataifa ikiendelea kunyamaza kimya?
Jumuiya ya Ulinganiaji wa Kiislamu ya Libya imeyataka mataifa, serikali na jumuiya za kisheria kote duniani kupaza sauti ya kupinga jinai zinazofanyika nchini Myanmar dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo na kutumia mbinu mbalimbali kulaani jinai hizo ikiwa ni pamoja na mbinu ya vikwazo vya kiuchumi. 1067246