Televisheni ya Press imeripoti kuwa kitengo cha utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mji wa Erzurum kimetangaza kuwa maonyesho hayo ya kazi za kisanii zinazohusiana na Qur'ani Tukufu yanafanyika kwa mnasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Karibu kazi 100 za kisanii zinazohusiana na Qur'ani zinaonyeshwa katika maonyesho hayo.
Ofisi ya kituo cha utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mji wa Erzurum pia imeandaa vikao vya kiraa ya Qur'ani Tukufu ambavyo vinahudhuriwa na makarii wa Kiirani na Kituruki. 1068272