IQNA

Myanmar yaruhusu misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Waislamu nchini humo

20:13 - August 11, 2012
Habari ID: 2390403
Serikali ya Myanmar imeziruhusu jumuiya za misaada ya kibinadamu za Kiislamu kuingia nchi humo kwa ajili ya kuwasaidia Waislamu wa jamii ya Rohingya.
Uamuzi huo ulichukuliwa katika kikao cha jana cha Rais Thein Sein wa Myanmar na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) katika mji mkuu wa zamani wa nchi hiyo Yangon.
Kikao hicho kilijadili hali ya maeneo ya Waislamu wa Myanmar na njia za kupeleka misaada kwa watu walioathiriwa na machafuko ya eneo hilo.
Katika kikao hicho pia ujumbe wa OIC ulimweleza Rais wa Myanmar kwamba ulimwengu mzima wa Kiislamu unafuatilia kwa makini hali ya kusikitisha ya Waislamu wa eneo la Arakan nchini Myanmar na kutangaza kuwa jumuiya hiyo iko tayari kutoa misaada ya dharura kwa Waislamu wa eneo hilo
Wakati huo huo ripoti zinaeleza kuwa vikosi vya usalama vya Myanmar na Mabudha wenye misimamo mikali wanaendelea kuchoma na kuteketeza nyumba za Waislamu wa kabila la Rohingya katika jimbo la Rakhin nchini humo. Mbali na kuchoma moto nyumba za Waislamu, vikosi vya usalama vikiungwa mkono na Mabudha waliofurutu ada vimeteketeza pia misikiti kadhaa.
Katika wiki za hivi karibuni maelfu ya Waislamu wa kabila la Rohingya wameuawa na makumi ya maelfu ya wengine kuachwa bila makazi kufuatia machafuko yaliyozuka mashariki mwa Myanmar. 1075987
captcha