IQNA

Katibu Mkuu wa OIC atuma salamu za rambirambi kwa Iran

16:02 - August 13, 2012
Habari ID: 2392056
Ekmeleddin Ihsanoglu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Kiislamu (OIC) ametoa taarifa akielelezea masikitiko yake kuhusiana na mtetemeko wa ardhi ulioikumba Iran hivi karibuni.
Katika taarifa hiyo Ihsanoglu amesikitishwa sana na ukweli kwamba tetemeko hilo limesababisha maafa na hasara kubwa kwa wakazi wa Azerbaijan Mashariki. Amesema masikitiko ya mkasa huo yanazidi kuongezeka kutokana na ukweli kuwa watu zaidi wanaendelea kupoteza maisha kutokana na athari za mtetemeko huo.
Katibu Mkuu huyo ametangaza masikitiko na maombolezo yake na serikali pamoja na taifa la Iran na hasa jamaa na familia za wahanga wa tukio hilo katika wakati huu mgumu. Amesema OIC iko tayari kutoa kila aina ya msaada wa kibinadamu kwa waathirika.
Amewapongeza viongozi wa serikali ya Iran kwa kuwashughulikia haraka waathirika wa mkasa huo. Kiongoi huyo wa OIC ameelezea matumaini yake kwamba watu wa Iran wataweza kuwa na subira na utulivu hasa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kwa ajili ya kukabiliana na athari za janga hilo. 1077296
captcha