Alitoa pendekezo hilo katika kikao cha nne cha dharura cha wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) katika mji mtakatifu wa Makka. Amesema wanachama wa kituo hicho ambao watakuwa na makao yao mjini Riyadh wanapasa kuchaguliwa na Katibu Mkuu wa jumuiya ya (OIC) na Kamati ya Mawaziri wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo. Amesema jukumu kuu la kituo hicho litakuwa ni kuzuia kuenea fitina na unafiki kati ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na Suni na kutafuta njia za kuimarisha ushirikiano kati ya wafuasi wa madhehebu mbili hizo.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake Mfalme Abdallah amesema kwamba hakuna kitu kibaya na hatari kama mfarakano katika umma wa Kiislamu na kusisitiza kwamba nchi za Kiislamu zinapasa kufanyajuhudi kubwa kwa lengo la kuimarisha umoja na mshikamano kati ya wafuasi wa madhehebu tofauti za Kiislamu.
Kikao cha nne cha dharura cha OIC ambacho kilianza mjini Makka siku ya Jumatatu tarehe 13 kinatazamiwa kukamilika hapo kesho Alkhamisi tarehe 16 Agosti. Kuchunguzwa hali ya nchi za Kiislamu na hasa matukio ya Syria na Mali ni ajenda muhimu ya kikao hicho.1079234