IQNA

Vipindi vya Haram ya Imam Hussein (as) vyarushwa hewani moja kwa moja

12:44 - August 16, 2012
Habari ID: 2394323
Vipindi vinavyoendeshwa katika Haram za Imam Hussein, Hadhrat Abul Fadhl katika mji mtakatifu wa Karbala na Haram ya Imam Ali (as) mjini Najaf vimekuwa vikirushwa hewani moja kwa moja kupitia kanali tofauti za Taasisi ya Idhaa na Televisheni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na hasa Kanali ya Qur'ani.
Akizungumzia suala hilo, Muhammad Muhammadi Mu'miniha, mkurugenzi wa ofisi za Taasisi ya Idhaa na Televisheni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika miji mitakatifu ya Iraq amesema jambo hilo limewezekana kufuatia safari ya hivi karibuni ya Ezzatollah Zarghami, mkuu wa taasisi hiyo katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala ambapo alitoa amri ya kuanzishwa ofisi hizo katika miji hiyo kwa shabaha ya kuakisiwa matukio na vipindi vya kidini vinavyotayarishwa katika miji hiyo.
Mu'miniha amesema kabla ya hapo vipindi vyote vilivyokuwa vikitangazwa kutoka miji hiyo vilikuwa vikitayarishwa na kurushwa hewani kutokea majengo yaliyo karibu na haram hizo na kwamba hii ni mara ya kwanza kwa vipindi kutayarishwa na kupeperushwa hewani moja kwa moja kutoka ndani ya haramu hizo na hasa pembenei ya makaburi ya watukufu hao. 1080010
captcha