Taarifa ya OIC imesema kuwa makubaliano na sheria zote za kimataifa hususan makubaliano ya Geneva yanaizuia Israel kushambulia maeneo matakatifu ya Quds Tukufu na utawala huo haupasi kuwazuia watu kutekeleza swala katika maeneo hayo.
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa Mayahudi wenye misimamo mikali wangali wanaendelea kushambulia viwanja vya Msikiti wa al Aqsa na kutoa wito wa kuvunjwa msikiti huo na kujenga mahala pake hekalu la Mayahudi. Imesisitiza kuwa Quds inakabiliwa na hujuma ya kibaguzi na lengo la mpango huo ni kuwafukuza wakazi asili wa eneo hilo katika mji huo.
Mwishoni mwa taarifa hiyo Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imeutaka umma wa Kiislamu kuchukua msimamo madhubuti wa kuilinda Quds Tukufu na utambulisho wake wa Kiarabu na Kiislamu.
Agosti 21 mwaka 1969 Myahudi aliyekuwa na misimamo mikali wa Israel Denis Michel aliichoma moto sehemu ya mashariki ya Msikiti Mtukufu wa al Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu, na kuteketeza vilivyokuwamo ikiwa ni pamoja na minbari ya kihistoria ya Salahuddin na kuba ya msikiti huo.
Wakati huo wananchi wa Palestina walifanya juu chini kuzima moto huo licha ya askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel kuwazuia. 1083055