IQNA

Imam Khamenei awapongeza wanamichezo wa Iran

16:31 - September 10, 2012
Habari ID: 2409092
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Imam Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amewashukuru washindi walioliletea taifa medali katika mashindano ya Paralympic yaliyomalizika jana mjini London, Uingereza.
Imam Ayatullah Khamenei ametoa shukurani za dhati kwa majeruhi wa vita na vilema wa Iran kwa kupata mafanikio makubwa katika michezo ya Paralympic ya London. Katika ujumbe wake kwa mashujaa hao Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: "Fakhari mliyopata katika mashindano ya kimataifa imelifurahisha taifa la Iran, na kwa dhati nakushukuruni nyote. Vilevile kushikamana kwenu na thamani na sheria za Kiislamu (katika mashindano hayo) kunastahiki pongezi na shukrani"
Timu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika michezo ya Paralympic mjini London imefanikiwa kujinyakulia medali 24 kwa ujumla zikiwemo dhahabu 10, fedha 7 na shaba 7 na kushika nafasi ya 11 ya mashindano hayo yaliyomalizika jana. 1095059
captcha