IQNA

Jumuiya ya Taqrib yalaani kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu

23:56 - September 15, 2012
Habari ID: 2412079
Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu imetoa taarifa ikilaani vikali kitendo cha kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad (saw) na kutangaza kuwa serikali za kibeberu zimedhihirisha udhaifu wao mbele ya nguvu inayoimarika kila siku ya Uislamu duniani kwa kutengeneza filamu hiyo ya kudhalilisha.
Taarifa hiyo imesema, kwa mara nyingine tena serikali za kibeberu zimedhihirisha udhaifu wao mbele ya nguvu inayoongezeka kila siku ya Uislamu katika Mashariki ya Kati na ulimwenguni kwa kutengeneza filamu inayiomvunjia heshima Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).
Imesema kuwa wahusika wa nyuma ya pazia katika kitendo hicho kichafu ni vibaraka wa Uzayuni na Marekani ambao wanataka kuzima mwamko wa Kiislamu na harakati za kupambana na ubeberu na kueneza harakati za kigaidi kwa jina la uhuru wa fikra na kujieleza.
Taarifa ya Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu imesisitiza kuwa Imam Khomeini Mwenyezi Mungu amrehemu alisema kweli kwamba hujuma dhidi ya matukufu ya Kiislamu ni siasa ya kistratijia ya pande tatu za Marekani, Wazayuni an Uingereza inayolenga kuzuia harakati za Kimapinduzi na za kupigania uhuru za Waislamu za kutaka kujiondoa kikamilifu chini ya makucha ya wakoloni na vibaraka wao wa ndani.
Taarifa hiyo imelaani vikali hujuma zinazolenga Uislamu za Marekani, Wazayuni na vinara wengine wa ubeberu wa kimataifa ambazo zimewakasirisha walimwengu hususan mamilioni ya Waislamu kote duniani na kutangaza kuwa mwamko wa kiislamu katika nchi za Waislamu umepinga kengele ya hatari kwa mabeberu kwamba tawala zote za kibeberu na Israel zitaangamizwa na kwamba jibu bora zaidi la jinai kama hizo ni umoja na mshikamano wa Kiislamu mbele ya ubeberu wa kimataifa. 1098430
captcha