IQNA

Vitabu vya Kiislamu vinauzwa kwa wingi Uingereza baada ya filamu inayomvunjia heshima Mtume (saw)

15:20 - September 23, 2012
Habari ID: 2417905
Wananchi wa Uingereza wanaelekea kwa wingi katika maduka ya kuuza vitabu vya Kiislamu kwa shabaha ya kutaka kuijua vyema dini tukufu ya Uislamu baada ya kuonyeshwa filamu inayomvunjia heshima Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad (saw).
Maduka ya kuuza vitabu nchini Uingereza yanaripoti kuwa, uuzaji vitabu vya Kiislamu umeongezeka kwa asilimia 30 nchini humo baada ya kutolewa filamu ya Innocence of Muslims inayomtusi Mtume Muhammad (saw).
Ripoti zinasema kuwa baada ya kutazama filamu hiyo ya Kimarekani Waingereza wasio Waislamu wamekuwa na hamu kubwa ya kuujua Uislamu na wamekuwa wakinunua kwa wingi vitabu vinavyohusiana na dini hiyo ya Mwenyezi Mungu.
Vilevile tarjumi ya lugha ya Kiingereza ya Qur’ani Tukufu ni miongoni mwa vitabu vinavyouzwa kwa wingi nchini humo. 1104763
captcha