IQNA

Maelfu waandamana Michigan dhidi ya filamu iliyo dhidi ya Uislamu

16:00 - September 30, 2012
Habari ID: 2423067
Maelfu ya wakaazi wa mji wa Michigan nchini Marekani wameandamana kulaani filamu ya Marekani pamoja na vijikatuni vinavyomvunjia heshima Mtume Mtukufu (saw) vilivyochapishwa hivi karibuni huko Ufaransa.
Kwa mujibu wa televisheni ya Press TV waandamanaji hao wamebeba mabango yaliyokuwa yameandikwa maandishi ya kulaani chuki na ubaguzi dhidi ya Uislamu na matukufu yake. Maandamano hayo yalipangwa na jumuiya pamoja na viongozi wa Marekani walio na asili ya nchi za Kiarabu na Asia.
Maandamano ya kupinga chuki na dharau dhidi ya matukufu ya Kiislamu yameongezeka duniani katika siku za hivi karibuni kufuatia hatua ya jarida moja la Ufaransa la kuchapisha vikatuni vya kumvunjia heshima Mtume mara tu baada ya kuonyeshwa duniani kupitia mtandao wa intaneti filamu iliyotengenezwa Marekani, inayomvunjia heshima Mtume Mtukufu (saw).
Waandamanaji ambao wamekuwa wakiandamana mbele ya balozi za Marekani katika pembe tofauti za dunia wamechoma moto bendera za nchi hiyo ili kudhihirisha chuki yao dhidi ya utawala wa nchi hiyo ulioruhusu kutengenezwa na kuonyeshwa filamu hiyo iliyo dhidi ya matukufu ya Kiislamu.
Vilevile wamekuwa wakitaka kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria na kuchukuliwa hatua kali wahalifu wote waliohusika na filamu hiyo.
Inasemekana kuwa Wazayuni walitoa mchango wa dola milioni tano za Marekani kusaidia utenegenezaji wake. 1110389
captcha