IQNA

Mamufti Russia wapongeza uamuzi wa mahakama

22:18 - October 02, 2012
Habari ID: 2424777
Baraza la Mamfuti katika eneo la Caucasus Kaskazini nchini Russia wamepongeza uamuzi wa makahama nchini kupiga marufuku filamu ya Marekani inayomkashifu Mtume SAW.
Mufti Shafiq Pshikhachev ambaye ni mwakilisi wa Baraza la Mamufti wa eneo la Caucasus Kaskazini mjini Moscow na Mwenyekiti wa Taasisi ya Utamaduni wa Kiislamu amesema: ‘Nataka kuishukuru mahakama kwa kupitisha uamuzi kama huo, ni hatua chanya katika kulinda haki za Waislamu.’
Hivi karibuni mahakama ya moja katika mji mkuu wa Russia, Moscow ilitangaza kuwa, ni marufuku nchini humo kuonyeshwa filamu iliyotengenezwa Marekani ambayo inamtusi na kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW.
Mahakama hiyo ilisema kwamba, filamu hiyo haipaswi kuonyeshwa nchini humo, kwani inamvunjia heshima Mtume SAW, na inapingwa na Waislamu kote ulimwenguni.
1112099
captcha