Sayyid Nasrullah amesema kuwa ndege hiyo iliingia magharibi mwa Mediterania kutoka Lebanon na baada ya kukata masafa ya mamia ya kilomita iliingia katika maeneo yanayokaliwa mabavu na utawala haramu Israel baada ya kuvuka vizingiti vingi karibu na eneo la Dimona lenye viwanda vya silaha za nyuklia za Israel ambako iliangushwa.
Ameashiria kuwa Waziri Mkuu wa utawala haramu Israel Benjamin Netanyahu ametangaza rasmi kwamba Hizbullah imehusika na operesheni hiyo na kuongeza kuwa, ndege hiyo isiyo na rubani imetengenezwa na wataalamu wa Hizbullah kwa kutumia teknolojia ya Kiirani.
Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema utengenezaji wa ndege hiyo iliyoingia katika maeneo ya kistratijia ya Israel na kupaa kwake katika anga ya maeneo muhimu ya Israel vimeonesha uwezo mkubwa wa Hizbullah. Amesema mafanikio hayo yanatokana na kuwa ndege hiyo imeweza kuingia katika maeneo yenye ulinzi mkali ya utawala haramu wa Israel. Ameongeza kuwa Hizbullah imechukua hatua hiyo kujibu ukiukaji wa anga ya Lebanon unaofanywa mara kwa mara na ndege za kivita za utawala haramu wa Israel.
1117802