Ijumaa tarehe 12 Agosti 2012, jeshi la Polisi mjini Dar es Salaam Tanzania lilitumia nguvu za ziada kutuliza ghasia baada ya kijana mmoja wa Kikristo anayejulikana kwa jina la Emmanuel Josephat kuutemea mate na kuukojolea Msahafu huko Mbagala na hivyo kuamsha hasira za Waislamu wenye uchungu na dini yao.
Imearifiwa kuwa polisi walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya Waislamu wenye hasira ambao walikuwa wanataka polisi iwakabidhi kijana huyo aliyeivunjia heshima Qur'ani Tukufu.
Makanisa kadhaa yalichomwa moto baada ya polisi kukataa kuwakabidhi Waislamu kijana huyo aliyevunjia heshima matukufu ya dini yao tukufu.
Waislamu kadhaa walikamatwa katika vurugu hizo na viongozi wa Kiislamu wametaka waachiliwe huru mara moja.
Bwana Hamis Salum Mzazi wa kijana ambaye alipokonywa Msahafu huo amenukuliwa akisema: Kijana wangu alikuwa anatoka Madrasa alipofika katika maeneo ambayo huwa wanapenda kucheza mpira akaja huyu kijana akamwambia wewe una mapepo, hii Qur'ani ni kitu gani, mnapoteza muda tu, kule kuna mashetani, majini na uchawi... halafu yule kijana akachukua Msaafu akaufunua wakatokea watoto wengine wakamwambia utadhurika, utageuka mjusi... akaufunua na kuutemea mate na kisha baadae akaukojolea"
Waislamu Tanzania wamesikitishwa na hatua ya rais Jakaya Kikwete wa nchi hiyo kutembelea makanisa yaliyoteketezwa moto pasina kulaani kitendo cha kuvunjia heshima Qur’ani Tukufu.
1120032