Rais Ahmadinejad ameyasema hayo katika mkoa wa Hormuzgan kusini mwa Iran Jumamosi usiku katika hafla ya kuwaenzi maafisa wa Jeshi la Wanamaji la Iran.
Rais Ahmadinejad ameongeza kuwa vikosi vya kigeni haviwezi kamwe kufanikiwa kuleta usalama katika Ghuba ya Uajemi.
Rais Ahmadinejad amelipongeza jeshi la wanamaji la Iran kwa uwezo wake mkubwa. Amesema kuwepo jeshi la wanamji la Iran katika maji ya kimataifa ni tukio muhimu katika historia ya nchi hii. Rais Ahmadinejad ameongeza kuwa taifa la Iran halijawahi kuwa na sera za kutaka kutawala nchi zingine lakini wakati huo huo historia inaonyesha kuwa taifa hili huwasambaratisha vibaya wavamizi.
1127304