Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran, Ayatullah Ahmad Khatami amelaani mashambulizi ya kinyama ya utawala haramu wa Israel katika ukanda wa Ghaza ambayo hadi sasa yameshasababisha kufa shahidi zaidi ya Wapalestina 20.
Ayatullah Khatami amesema mikono ya Wazayuni imejaa damu na kwamba utawala huo umejengeka juu ya misingi ya unyama, ukatili na udhalimu. Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran aidha amewapongeza wanamapambano wa Palestina kwa kusimama kidete na kujibu mashambulizi ya Wazayuni. Amesema Uislamu unamtaka kila Muislamu kutetea haki yake na kujilinda vilivyo wakati anapovamiwa. Huku hayo yakijiri, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Ali Akbar Salehi amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuunga mkono juhudi za wanamapambano wa Palestina za kulinda ardhi yao mbele ya uchokozi na chokochoko za utawala haramu wa Israel. Salehi amesema hayo alipozungumza kwa njia ya simu na Ramadhan Abdallah, Katibu Mkuu wa Jihadul Islami ya Palestina.
1138327