Kongamano hilo litaongozwa na Profesa Muhammad Abdulhalim ambaye ni mtarjumi wa Qur'ani Tukufu na Helen Blatherwick, mhadhiri wa fasihi ya lugha ya Kiarabu katika Chuo Kikuu cha London.
Kongamano hilo limepangwa kufanyika tarehe 20 hadi 22 Novemba na litachunguza utafiti wa matini ya Qur'ani, tafsiri na tarjumi za kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.
Lengo la kongamano hilo ni kuchunguza masuala mbalimbali yanayohusu matini, tafsiri na tarjumi ya Qur'ani.
Makala zitakazochaguliwa katika kongamano hilo zitachapishwa katika jarida la utafiti wa Qur'ani la Chuo Kikuu cha London. 1206149