IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Uchaguzi wa rais wa Iran, hamasa itakayowashangaza walimwengu

19:13 - April 13, 2013
Habari ID: 2518676
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, uchaguzi ujao wa rais nchini Iran utafanyika kwa hamasa na mahudhurio makubwa na kuwashangaza tena walimwengu.
Ayatullah Muhammad Ali Movahedi Kermani amesema hayo mbele ya hadhara kubwa ya waumini waliohudhuria ibada ya Sala ya Ijumaa mjini Tehran na kusisitiza kwamba, wananchi wa Iran watajitokeza tena kwa wingi katika uchaguzi ujao wa rais uliopangwa kufanyika hapa nchini mwezi Juni mwaka huu na hivyo kuwakatisha tamaa kwa mara nyingine maadui wa taifa hili. Khatibu Movahedi Kermani amesema, uchaguzi ujao wa rais utakuwa fursa nyingine kwa wananchi wa Iran kutoa majibu kwa mashinikizo, propaganda chafu na njama za maadui dhidi ya taifa hili. Ayatullah Kermani sambamba na kuashiria maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni mjini Bushehr hapa Iran na kuzipa mkono wa pole familia zilizopoteza ndugu zao, amewapongeza maafisa wa serikali kutokana na kuharakisha shughuli za utoaji misaada katika eneo hilo.
1208002
captcha