IQNA

Nchi 58 kushiriki fainali za Mashindano ya 42 ya Kimataifa ya Qur’ani nchini Iran

16:27 - May 21, 2026
Habari ID: 3482266
IQNA – Hatua ya fainali ya Mashindano ya 42 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yatafanyika kwa ushiriki wa wawakilishi kutoka nchi 58, afisa mmoja amesema.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran siku ya Jumatano, Mkuu wa Kituo cha Masuala ya Qur’ani cha Shirika la Wakfu na Mambo ya Hisani, Hujjat‑ul‑Islam Seyed Nassereddin Nourizadeh, amesema hatua ya awali iliandaliwa kwa njia ya mtandao ambapo nchi 104 zilionesha utayari wao wa kushiriki, na hatimaye wawakilishi kutoka nchi 58 wakafuzu kufika hatua ya mwisho.

Amebaini kuwa kutokana na matukio muhimu yaliyotokea nchini, ikiwemo Vita vya Tatu Vilivyolazimishwa (Vita vya Ramadhani au uchokozi wa Marekani na Israel dhidi ya Iran) pamoja na njama za maadui, na pia kutokana na kufariki kishahidi kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei pamoja na wenzake, hatua ya fainali ya mashindano hayo iliahirishwa.

Head of the Quranic Affairs Center of Iran’s Awqaf and Charity Affairs Organization Hojat-ol-Islam Seyed Nassereddin Nourizadeh

Hata hivyo, kwa uamuzi wa mkuu wa shirika la kuendeleza programu za Qur’ani kwa uzito zaidi, fainali hizo zimepangwa kufanyika upya Juni–Julai mwaka huu, ameongeza mwanazuoni huyo.

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huandaliwa kila mwaka na Shirika la Iran la Wakfu na Mambo ya Hisani.

Mashindano hayo yanalenga kukuza utamaduni na maadili ya Qur’ani miongoni mwa Waislamu, pamoja na kuonesha vipaji vya wasomaji na wahifadhi wa Qur’ani Tukufu.

Habari zinazohusiana
captcha