IQNA

Maonyesho ya tarjumi za Qur'ani kwa lugha mbalimbali Zimbabwe

13:55 - April 18, 2013
Habari ID: 2520694
Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu nchini Zimbabwe kinaonyesha tafsiri na tarjumi ya Qur'ani Tukufu kwa lugha mbalimbali katika maonyesho ya vitabu yanayofanyika nchini humo.
Vilevile vitabu vinavyohusu Uislamu na Ahlul Bait (as) vimewekwa katika maonyesho hayo.
Katika maonyesho hayo ya siku tatu yanayofanyika Bulawayo, Kitengo cha Utamaduni cha Iran kina vyumba viwili kimoja cha maonyesho ya vitabu vinanyohusu Uislamu na kingine kinaonyesha vitabu kuhusu Iran.
Vitabu vya Marehemu Ayatullah Musavi Lari, jografia, historia, utamaduni, sanaa na maendeleo ya Iran ya Kiislamu pia vinaonyeshwa katika maonyesho hayo. 1214175
captcha