IQNA

Qur'ani yavunjiwa heshima katika jela ya Saudi Arabia

13:55 - April 18, 2013
Habari ID: 2520695
Kundi la vijana wa Kisaudi Arabia limefanya maandamano katika mji wa al Qassim likilaani kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika jela ya wafungwa wa kisiasa ya al Hair.
Vijana hao wamelaani vikali kitendo cha maafisa wa jela ya al Hair cha kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu. Waandamanaji hao wametoa wito wa kufikishwa mahakamani maafisa wa jela hiyo waliovunjia heshima Qur'ani, kufutwa kazi Waziri wa Mambo ya Ndani wa Saudia Muhammad bin Nayif na kuachiwa huru wafungwa wote wanaoshikiliwa katika jela hiyo.
Wafungwa wanaoshikiliwa katika jela hiyo wamewaambia jamaa zao kwamba maafisa wa jela wamerusha chini na kuzipiga teke nakala za Qur'ani Tukufu kwa shabaha ya kuchochea hisia za wafungwa hao.
Askari usalama wa serikali ya Saudia walipelekwa katika jela ya Hair baada ya wafungwa wa jela hiyo kupinga kitendo cha kuvunjiwa Qur'ani Tukufu. 1213793
captcha