Maliki ameyasema hayo siku ya Jumamosi alipohutubua Kongamano la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu ambalo limefanyika katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad.
Watu zaidi ya 200 wameuawa katika wimbi jipya la machafuko ambalo lilianza Iraq Jumanne iliyopita.
Waziri Mkuu wa Iraq ametoa wito kwa wasomi wa Kiislamu wanaoshiriki katika kikao hicho kujaribu kutafuta sulushisho la machafuko ya Iraq.
Al Maliki amezituhumu nchi jirani za Saudi Arabia na Qatar kuwa ndio chanzo cha uchozezi wa machafuko ya kimadhehebu nchini humo.
1219017