IQNA

Iran kusambaza nakala milioni moja za Qur'ani duniani

23:03 - July 07, 2013
Habari ID: 2557817
Waziri wa Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu wa Iran amesema Iran iko tayari kusambaza nakala milioni moja za Qur'ani baina ya Waislamu katika nchi mbalimbali duniani.
Dkt. Sayyed Mohammad Husseini ameyasema hayo pembizoni mwa sherehe za kufungua Maonyesho ya 21 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu mjini Tehran na kuongeza kuwa nakala hizo za Qur'ani zitakazosambazwa kote duniani zimechapishwa katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Amesema maoneysho hayo ndio muhimu zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu kwa mtazamo wa idadi ya wanaotembelea maonyesho, athari zinazoonyeshwa na viwango vya bidhaa za Qur'ani.

Dkt. Husseini ametoa wito kwa Waislamu wa madhehebu zote na hata wasiokuwa Waislamu kuyatembelea maonyesho hayo ambayo yataendelea kwa muda wa mwezi moja. Maonyesho ya 21 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yalifunguliwa Ijumaa mjini Tehran na Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Maonyesho hayo ya kimataifa yameanza alasiri ya jana katika uwanja mkubwa wa swala wa Imam Khomeini.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani mwaka huu yana vitengo 40 vikiwemo vya majarida ya Qur'ani, vyuo vikuu vya kidini na visivyo vya kidini, tarjumi ya Qur'ani Tukufu, Qur'ani, Vijana na watoto, mwenendo wa maisha ya Kiqur'ani, Qur'ani na dini mbalimbali, Qur'ani na sayansi, Qur'ani na umoja wa Kiislamu na kadhalika.
1250001
captcha