Mkuu wa Kituo cha Masuala ya Qur'ani Tukufu cha Taasisi ya Wakfu na Masuala la Kheri cha Iran amesema kuwa, mahafali 420 ya kuwa na mapenzi na ukuruba na Qur'ani Tukufu yatafanyika katika pembe mbalimbali za Iran yakiwashirikisha maqarii 8 bingwa wa Misri na yataendelea katika siku zote za mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Bw. Waliyullah Yar Ahmadi ametangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, maqarii hao wa Misri watakuwa wanatembelea mikoa mbalimbali ya Iran kwa ajili ya kusoma Qur'ani Tukufu katika mahafali hayo yatakayojumuisha masuala mbalimbali yanayohusiana na Qur'ani.
Amewataja maqarii hao bingwa wa Misri kuwa ni pamoja na Ustadh Mahmoud Siddiq Manshawi, Ustadh Walid Yahya Raghib Sharqawi, Ustadh Ali Mahmoud Shamis, Ustadh Faruq Ahmad Dhif, Ustadh Adil al Baz na Ustadh Ahmad Shahat Ahmad Sayyid.
Mahafali ya Qur'ani tukufu ni jambo la kawaida nchini Iran na huwa yanapata nguvu sana hapa nchini katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
1257749