Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa, kuimarishwa umoja kati ya umma wa Kiislamu ni njia pekee ya kuweza kukabiliana na njama za Marekani na waitifaki wake kote duniani khususan katika umma wa Kiislamu.
Ameyasema hayo katika mazungumzo na Ayatullah Muhsin Araqi Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuyakurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu.
Sayyid Hassan Nasrullah ameashiria njama za hivi karibuni za kupenda vita za Marekani, utawala wa Kizayuni na waitifaki wao na kueleza kuwa matukio ya kieneo hayapasi kusahaulisha jinai dhidi ya binadamu zinazofanywa kila uchao na utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya wananchi madhlumu wa Palestina.
Katika mazungumzo hayo, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon pia ameitaja kuwa hatua muhimu kufunguliwa huko Lebanon ofisi ya mwakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuyakurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu. Kwa upande wake, Ayatullah Muhsin Araqi, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuyakurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu amesema, kuna udharura wa kukuribiana madhehebu za Kiislamu na kuongeza kuwa, utawala wa Kizayuni unaoikalia Quds tukufu kwa mabavu ni adui wa watu wote wa eneo hili na Waislamu wa madhehebu yote.
1287424