IQNA

Qarii mkubwa wa Qur'ani wa Misri afariki dunia

19:20 - September 18, 2013
Habari ID: 2591914
Sheikh Mahmoud Amin Tantawi ambaye alikuwa miongoni mwa maqarii wakubwa wa Qur'ani alifariki dunia jana mjini Cairo.
Sheikh Amin Tantawi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Qur'ani katika Chuo Kikuu cha al Azhar alifariki dunia jana akiwa nyumbani kwake na kuzikwa kijijini alikozaliwa katika mkoa wa al Sharqiyya.
Msomaji huyo mkubwa wa Qur'ani alizaliwa tarehe 30 Novemba mwaka 1930 na alikuwa Naibu Mwenyekiti wa Kitengo cha Maqarii wa Qur'ani Tukufu wa Misri. Sheikh Amin Tantawi ndiye qarii pekee aliyeshiriki kwa kipindi cha miaka 22 katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani la Malaysia kama mwamuzi.
Alihifadhi Qur'ani nzima kabla ya kutimiza umri wa miaka 10 na kukamilisha masomo ya sheria za Qur'ani akiwa na umri wa miaka 11 na kuingia katika chuo cha qiraa ya Qur'ani. Aliendelea kusoma kwenye chuo hicho hadi mwaka 1960.
Sheikh Tantawi ameandika vitabu kadhaa katika taaluma ya qiraa na sayansi ya Qur'ani. 1290289
captcha