Kituo cha Uhakiki wa Kiislamu cha al Azhar kimetangaza kuwa, katika nakala hizo zilizopotoshwa za Qur'ani Tukufu zinazooneshwa kwenye mitandao ya intaneti kunaonekana aya kadhaa zilizopotoshwa ikiwa ni pamoja na kuongezwa neno «الحق» mara tatu mtawalia katika aya ya 7 ya Suratu Aal Imran kwa sura ifuatayo:
"هُوَ الَّذِیَ أَنزَلَ عَلَیْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آیَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ فَأَمَّا الَّذِينَ فی قُلُوبِهِمْ زَیْغٌ فَیَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ (بالحق بالحق بالحق) مِنْهُ"
Hii ni katika hali ambayo aya hiyo ya Suratu Aal Imran haina neno hilo.
Sheikh Taufiq Abdul Aziz ambaye ni Katibu wa Kituo cha Uhakiki wa Kiislamu cha al Azhar ametoa taarifa akiwataka watumiaji wa mitandao ya intaneti kurejea katika mitandao yenye itibari na inayoheshimika kwa ajili ya kusoma Qur'ani Tukufu.
Vilevile ameyataka mashirika yanayojihusisha na masuala ya Qur'ani kwenye mitandao ya intaneti kuwa angalifu sana kabla ya kuweka nakala za Qur'ani, Hadithi na masuala mengine yanayohusiana na taaluma za Kiislamu.
Awali watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Facebook walitoa habari ya kuwepo nakala zilizopotoshwa za Qur'ani katika mtandao wa intaneti na kusema nakala hizo za Qur'ani zina maneno ya nyongeza au zina mapungufu ya baadhi ya aya. 1293328