IQNA

Waliochoma Qur'ani Kuwait watakiwa kufikishwa mahakamani

20:40 - October 22, 2013
Habari ID: 2607277
Mwanaharakati wa kisiasa wa Kuwait Hamoud Mubarak al Azmi ametoa wito wa kufikishwa mahakamani watu waliotenda jinai ya kuchoma moto nakala ya kitabu kitukufu cha Qur'ani katika msikiti wa eneo la Salimiyya nchini humo.
Mubarak al Azmi amelaani vikali kitendo cha kuchomwa moto nakala ya Qur'ani Tukufu na ameitaka Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo kuwatia nguvuni na kuwafikisha mahakamani waliofanya kitendo hicho.
Hamoud al Mubarak amesema kuwa kitendo hicho kimefanywa na wajinga wanaotaka kuzusha fitina nchini Kuwait na kwamba wahusika wamekivunjia heshima kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.
Mwanaharakati huyo wa kisasa pia ameitaka serikali ya Kuwait na Bunge la nchi hiyo kutunga sheria inayolaani na kuwaadhibu watu wanaovunjia heshima matukufu ya Kiislamu. 1306257
captcha