IQNA

Matokeo ya awali ya mashindano ya Qur'ani Kuwait yatangazwa

20:19 - October 28, 2013
Habari ID: 2609669
Matokeo ya awali ya mashindano ya 17 ya taifa ya Qur'ani Tukufu nchini Kuwait katika taaluma za tajwidi na hifdhi ya Qur'ani yalitangazwa jana katika kikao kilichohudhuriwa na Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa nchi hiyo.
Gazeti la Kuwait News limeripoti kuwa, Waziri wa Wakfu wa nchi hiyo Shareeda Al- Muosherji alitangaza matokeo ya mashindano hayo jana na kusema kuwa, mashindano ya taifa ya Qur'ani yana nafasi makhsusi nchini Kuwait kati ya mashindano mengine ya Kiislamu na ya Qur'ani yanayofanyika nchini humo. Amesema mashindano hayo yanafanyika kwa ajili ya kushajiisha vijana kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu. Ameongeza kuwa lengo jingine ni kuonesha umuhimu wa kitabu hicho kitukufu kwa vizazi vijavyo.
Kwa upande wake Katibu wa Wizara ya Wakfu ya Kuwait Abdul Muhsin al Kharrafi amesema kuwa maqarii 1761 kati ya watu 2640 walioshiriki katika mashindano hayo waliingia katika duru ya mwisho na kwamba 155 kati yao wameingia fainali.
Awamu ya mwisho ya mashindano ya taifa ya Qur'ani Tukufu nchini Kuwait itafanyika kuanzia tarehe 30 Oktoba hadi Novemba 2. 1309109


captcha