Maonyesho hayo yanasimamiwa na kamati ya maandalizi ya Tamasha la Kimataifa la Ghadir na yatafanyika katika Haram ya Imam Ali bin Abi Twalib (as) mjini Najaf.
Katika maonyesho hayo ya siku tatu kutaoneshwa nakala za Qur'ani Tukufu zilizoandikwa kwa hati za mkono katika karne ya kwanza hadi ya nne Hijria.
Msimamizi wa maonyesho hayo ya Qur'ani amesema maandalizi yanaendelea ndani ya Haramu ya Imam Ali (as) na kwamba nakala za Qur'ani Tukufu zilizoandikwa kwa hati za mkono na zilizopambwa kwa maji ya dhahabu zitaonyeshwa katika shughuli hiyo.
Hashim Muhammad Murtadha amesema msahafu unaonasibishwa kwa Imam Ali bin Abi Twalib (as) ambao uliandikwa mwaka 40 Hijria pia utaonyeshwa katika maonyesho hayo ya Qur'ani. 1308844