IQNA

Nakala za Qur'ani zaendelea kununuliwa zaidi Ufaransa

16:58 - February 04, 2015
Habari ID: 2809494
Idadi ya nakala za Qur'ani Tukufu zilizouzwa nchini Ufaransa baada ya mashambulizi ya kigaidi yaliyolenga ofisi za jarida la kila wiki la Charlie Hebdo lililochapisha vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) imeongezeka kwa kiasi kikubwa.

Duka la kuuza vitabu ya La Procure mjini Paris imeripoti kuwa, idadi ya nakala za Qur'ani zilizouzwa katika siku za baada ya mashambulzi hayo imeongeza ghafla.
Afisa wa masuala ya kidini wa duka hilo la kuuza vitabu amesema hii ni mara ya kwanza kushuhudiwa ongezeko kubwa kiasi hiki cha ununuzi wa idadi kubwa zaidi ya nakala a Qur'ani.
Amesema wakati wa kurushwa hewani filamu ya matukio ya kweli ya Watawa wa Tibhirine (Monks of Tibhirine) inayohusu watawa saba wa Kifaransa waliouawa na makundi ya kigaidi katika mkoa wa Medea nchini Algeria mwaka 1996, idadi ya ununuzi wa vitabu vinavyohusu Uislamu na uhusiano wa Waislamu na Wakristo iliongezeka lakini hii ni mara ya kwanza kuongezeka ununuzi wa nakala za Qur'ani. AIR

2762200

captcha