IQNA

Qatar yaandaa maonyesho ya miujiza ya Qur'ani

16:40 - June 25, 2015
Habari ID: 3318504
Qatar imeandaa maonyesho kuhusu miujiza ya Qur'ani Tukufu na mafanikio ya wanasayansi Waislamu katika historia.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maonyesho hayo yenye anuani ya 'Miujiza na Mafanikio' yameandaliwa na Taasisi ya Utamaduni ya Qatar katika mji mkuu wa nchi hiyo, Doha.
Maonyesho hayo yana vitengo  vitano vinavyolenga kuhimiza kutafakuri kuhusu miujiza ya Qur'ani sambamba na kuarifisha mafanikio ya wanasayansi Waislamu. Sehemu ya kwanza inajumuisha aya za Qur'ani zilizoambatana na picha zenye taswira za maajabu ya maumbile yaliyotajwa katika Qur'ani.  Sehemu ya pili inawaarifisha wanasayansi 20 maarufu Waislamu ambao waliweza kufanya uvumbuzi katika sekta mbali mbali. Katika sehemu ya tatu wasomi na maulamaa wa Kiislamu wamearifishwa huku sehemu za nne na tano zikiwa ni maonyesho ya kaligrafia, nyaraka na vitabu nadra na vya kale.../mh

3318164

captcha