Taarifa iliyotolewa na Muungano wa Waislamu nchini humo imesema kesi za wanaharakati hao zimetiwa chumvi kutokana na misimamo yao dhidi ya dhulma za serikali kwa WaislamuWanaharakati hao 18 walishtakiwa mwezi uliopita kwa tuhuma kadhaa likiwemo suala la ugaidi na njama ya kubuni taifa la Kiislamu. Wamekana mashtaka hayo na kulalama kwamba walinyanyaswa wakati walipokuwa kizuizini. Wakati wa ziara ya rais Barack Obama nchini humo, baadhi ya wanaharakati walimueleza kuhusu kesi hiyo ambapo inadaiwa aliitaka serikali ya Addis Ababa iwaachilie huru.