Kozi hiyo imeanza wiki hii katika mji wa Najaf, kwa ushiriki wa wawakilishi kutoka nchi tano za Kiislamu, kwa mujibu wa Al-Kafeel.
Imeandaliwa ndani ya mpango wa Qur’ani kwa wanafunzi wa elimu za kidini kwa mwaka wa Hijria 1447.
Sheikh Mahdi Qalandar al-Bayati, mmoja wa wakufunzi wa kozi hiyo, alisema kuwa baraza hilo limeanzisha kozi ya tatu ya kuwaandaa maqari kwa kutumia mbinu za Iraq na Misri, kwa ushiriki wa wawakilishi 27 kutoka Iraq, Iran, Pakistan, Tanzania na Afghanistan.
“Kozi hii inajumuisha programu ya mafunzo ya kina chini ya usimamizi wa wataalamu,” alibainisha.
Al-Bayati aliongeza kuwa mtaala unalenga kuimarisha uwezo wa sauti wa washiriki na kukuza ustadi wao wa mitindo ya sauti, sambamba na mafunzo ya vitendo katika mbinu za hali ya juu za usomaji wa Qur’ani, ili kuwastawisha kwa ajili ya kushiriki katika mikusanyiko rasmi ya Qur’ani na vipindi vya usomaji.
Alifafanua kuwa kozi hiyo ina hatua mbili: ya kwanza ni hatua ya utangulizi inayowatambulisha washiriki kwa misingi ya usomaji na viwango vya utendaji, na ya pili ni hatua maalum inayochimbua uzoefu wao na kuongeza kiwango cha umahiri ili kuwataayarisha kushiriki katika programu za Qur’ani katika haram tukufu, misikiti, husseiniyya (maeneo ya kidini), na shule za kidini ndani na nje ya Iraq.