IQNA

Yemen yaendeleza oparesheni za kijeshi dhidi ya utawala katili wa Israel

15:22 - September 26, 2025
Habari ID: 3481288
IQNA-Jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel limesema ndege isiyo na rubani iliyorushwa kutoka Yemen imeshambulia mji wa kusini wa Eilat na kujeruhi watu 22 wakiwemo wawili ambao hali zao ni mahututi. Hayo yanajiri wakati jeshi la kizayuni likiwa lingali linaendeleza vita vyake vya kinyama na mauaji ya kimbari ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.

Taarifa ya jeshi la Israel imesema, ndege hiyo "iliangukia katika eneo la Eilat" kwenye pwani ya Bahari Nyekundu Jumatano baada ya mfumo wa ulinzi wa anga wa utawala huo kushindwa kuizuia.

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Yemen ya Ansarullah imetangaza rasmi kuwa ndiyo iliyohusika na shambulio hilo.

"Operesheni hiyo ilifanywa na idadi kadhaa ya ndege zisizo na rubani na kufanikiwa kulenga shabaha yake," ameeleza msemaji wa Vikosi vya Ulinzi vya Yemen Brigedia Jenerali Yahya Saree.

Saree amefafanua kwa kusema: "tumeshambulia maeneo kadhaa ya adui Israel katika maeneo ya Umm al-Rashrash na Bir al-Saba".

Kwa mujibu wa duru za habari, hii si mara ya kwanza kwa mji wa Eilat kushambuliwa na vikosi vya ulinzi vya Yemen. Wiki iliyopita pia ndege nyingine isiyo na rubani ya Yemen ilishambulia mji huo na mfumo wa ulinzi wa anga wa utawala wa kizayuni ulishindwa kuitungua.

Harakati ya Ansarullah ya Yemen imeapa kuwa haitasitisha mashambulizi dhidi ya maeneo ya utawala wa kizayuni katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu iliyopachikwa jina bandia la Israel, hadi pale utawala huo utakapositisha vita dhidi ya Ghaza, ambavyo hadi sasa vimeshapelekea zaidi ya Wapalestina 65,500 kuuawa shahidi. Vita hivyo vilivyoanzishwa Oktoba 2023 na Israel dhidi ya Wapalestina wa Ghaza vimetambuliwa rasmi na jopo la uchunguzi la Umoja wa Mataifa kuwa ni mauaji ya kimbari.

4306969

Habari zinazohusiana
captcha