IQNA

Watu wanne wauawa katika maandamano kizazi cha Gen-Z eneo la Waislamu wengi la Ladakh, India

14:14 - September 26, 2025
Habari ID: 3481283
IQNA – Waandamanaji wamepambana na vikosi vya usalama vya India katika jimbo lenye Waislamu wengi la Ladakh siku ya Jumatano, na ripoti zikisema angalau waandamanaji wanne wameuawa.

Ladakh, eneo lenye baridi katika milima ya Himalaya ambalo limekuwa kiini cha mvutano wa hivi karibuni kati ya India na China, liliathirika Jumatano na maandamano ya kizazi cha Gen-Z yaliyogeuka kuwa ya vurugu huku vijana wakiteketeza ofisi ya chama cha Bharatiya Janata Party (BJP) cha Waziri Mkuu wa India Narendra Modi.

Waandamanaji, wakiwemo wanafunzi, walipambana na polisi katika mji mkuu wa mkoa, Leh. Kwa mujibu wa waratibu wa maandamano angalau watu wanne waliuawa na kadhaa kujeruhiwa, kufuatia kuongezwa kwa majeshi ya silaha. Mamlaka zilisema makumi ya askari wa usalama pia walijeruhiwa kwenye mapambano hayo.

Kwa miaka sita iliyopita, maelfu ya watu wa Ladakh wakiongozwa na mashirika ya kiraia ya ndani, wamekuwa wakifanya maandamano ya amani na migomo ya kula ili kudai ulinzi mkubwa wa kikatiba na hadhi ya jimbo kutoka serikali kuu ya India, ambayo imekuwa ikitawala eneo hilo moja kwa moja tangu 2019. Wanataka nguvu ya kuchagua serikali ya eneo lao.

Hata hivyo, Jumatano, vikundi vya vijana waliokata tamaa viliachana na njia hizo za maandamano ya amani, alisema Sonam Wangchuk, mwalimu ambaye ameongoza mfululizo wa migomo ya kula.

Mnamo 2019, serikali ya Modi iliondoa kwa upande mmoja hadhi ya jimbo na uhuru wa nusu uliokuwa ukifurahiwa na Kashmir inayotawaliwa na India chini ya katiba ya India.

Jimbo hilo lilikuwa na maeneo matatu – Bonde la Kashmir lenye Waislamu wengi, Jammu lenye Wahindu wengi, na Ladakh ambako Waislamu na Wabudha kila mmoja wako takriban asilimia 40 ya idadi ya watu.

Baada ya hapo, serikali ya Modi ililigawa jimbo hilo la zamani kuwa maeneo mawili: Jammu na Kashmir yenye bunge, na Ladakh bila bunge. Wote wanaongozwa na serikali ya shirikisho na hakuna hata mmoja mwenye mamlaka kamili ya majimbo mengine nchini India, lakini bunge la Jammu na Kashmir angalau linawezesha wananchi kuchagua viongozi wa eneo la wakilisha maslahi yao New Delhi. Jimbo la Ladakh, wanasema wenyeji, halina hata haki hiyo.

Kashmir ni eneo lenye mzozo kati ya India, Pakistan na China – majirani watatu wenye silaha za nyuklia, kila mmoja anadhibiti sehemu yake. India inadai eneo lote, na Pakistan inadai lote isipokuwa sehemu inayoshikiliwa na China, mshirika wake. Kashmir inayotawaliwa na India inapakana na Pakistan upande wa magharibi, na Ladakh ina mpaka wa kilomita 1,600 (maili 994) na China kwa upande wa mashariki.

3494753

Kishikizo: kashmir india bjp
captcha